TANZANIA LOCAL GOVERNMENT WORKERS UNION

Talgwu Chama imara, huduma bora kwa wanachama

Dhima yetu

Kuunganisha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa kwa ajili ya kupigania uwepo wa huduma bora, uboreshwaji wa huduma za kiuchumi na kijamii, uwepo wa maendeleo endelevu ya kitaaluma na kitaalam, na kuimarisha nguvu ya pamoja ya majadiliano, ili kufikia kuwa jamii yenye usawa kupitia Uongozi bora

Dira yetu

Kuwa Chama cha Wafanyakazi chenye ufanisi mkubwa  na kinachojitegemea nchini Tanzania.

TALGWU ni nini?

Ni Chama cha wafanyakazi wa serikali za Mitaa Tanzania ambacho kimesajiliwa chini ya sheria ya vyama vya wafanyakazi no 10 ya mwaka 1998, na kilipewa nambari ya usajili  010 tarehe 15/09/2000. TALGWU inaunganisha wafanyakazi wote waliopo chini ya Mamlaka za serikali za mitaa na Taasisi nyingine  nchini ambapo hadi kufikia June 2024, Chama kilikuwa na wanachama 89,100.

TALGWU inajishirikisha na shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) ,shirikisho la vyama vya wafanyakazi vinavyotoa huduma kwa umma duniani (PSI) na Mtandao wa Vyama vya Wafanyakazi vya Serikali za Mitaa  Africa (AMALGUN). Hivyo basi chama cha wafanyakazi ni ummoja, muungano, na mshikamano wa wafanyakazi ambao nia, malengo, matakwa na matarajio yao yanafanana. Umoja huo ndio nguzo pekee ya kupatia ufumbuzi wa matatizo yao.

TALGWU inaelimisha, inatetea, na kulinda ajira na ujira wa wanachama wake kwa kuzingatia sheria, taratibu, kanuni, miongozo na nyaraka mbalimbali za kazi.

Je madhumuni ya kuanzishwa TALGWU ni yapi?

  • Kupigania na kuwahimiza waajiri kuboresha na kuendeleza hali nzuri ya wanachama katika maisha yao wakiwa kazini na wakati wa kustaafu.
  • Kujadiliana na kuondoa tofauti zinazojitokeza kati ya waajiri na wanachama, au mwanachama mmoja na mwingine kwa njia ya majadiliano/makubaliano ya amani kila itakapowezekana.
  • Kusimamia na kushauri katika uundaji wa mikataba ya hari bora mahali pa kazi.
  • Kuwaelimisha wanachama katika kuelewa sheria, kanuni na taratibu za nidhamu zinazotumika nchini.
  • Kuwasiliana na serikali kuhusu haja ya kutunga sheria sahihi za kazi na kuandaa sera nzuri za kuendeleza uchumi na maisha ya jamii.
  • Kulinda maslahi ya wanachama kwa kuwasiliana na serikali ili kuepukana na uandaaji wa sera ambazo ni hatari kwa wanachama.
  • Kuishauri Serikali kupunguza kodi ya mishahara ya mfanyakazi.
  • Kuishauri Serikali kurekebisha na kutengeneza Miundo ya Utumishi wa Umma ambayo haiwaumizi Wanachama wetu

Kwanini wafanyakazi wa Serikali za Mitaa wajiunge na TALGWU?

  • Ili kuwa na umoja katika kupigania haki na maslahi yao.
  • Kupata uwakilishi katika vyombo vya maamuzi.
  • Kupata msaada wa kisheria pale wanapokumbwa na migogoro kazini.
  • Kuelimishwa kuhusu masuala mbalimbali ya kiutumishi.
Scroll to Top