TALGWU ni Chama cha wafanyakazi wa serikali za Mitaa Tanzania ambacho kimesajiliwa chini ya sheria ya vyama vya wafanyakazi no 10 ya mwaka 1998, na kilipewa nambari ya usajili 010 tarehe 15/09/2000. TALGWU inaunganisha wafanyakazi wote waliopo chini ya Mamlaka za serikali za mitaa na Taasisi nyingine nchini ambapo hadi kufikia June 2024, Chama kilikuwa na wanachama 89,100.
TALGWU inajishirikisha na shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) shirikisho la vyama vya wafanyakazi vinavyotoa huduma kwa umma duniani (PSI) na Mtandao wa Vyama vya Wafanyakazi vya Serikali za Mitaa Africa (AMALGUN). Hivyo basi chama cha wafanyakazi ni ummoja, muungano, na mshikamano wa wafanyakazi ambao nia, malengo, matakwa na matarajio yao yanafanana.
Umoja huo ndio nguzo pekee ya kupatia ufumbuzi wa matatizo yao. TALGWU inaelimisha, inatetea, na kulinda ajira na ujira wa wanachama wake kwa kuzingatia sheria, taratibu, kanuni, miongozo na nyaraka mbalimbali za kazi
Waliopo hapo ni wajumbe wa Baraza, Wastaafu Viongozi wakuu wa Chama pamoja na Mgeni Rasmi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana,Ajira na wenye Ulemavu) Ndg Patrobas Paschal Katambi, waliohudhuria Kikao cha Baraza Kuu Taifa kilichofanyika Januari 2024 Jijini Dodoma
Mitandao
Huduma tunazotoa
Sheria
Kuwatetea wafanyakazi katika migogoro, mashauri na kesi mbali mbali pindi wanapokuwa kazini
Uwakilishi
Kuwawakilisha Wafanyakazi katika majadiliano ya pmoja na Serikali /Waajiri
Elimu
Kuwaelimisha Wanachama kuhusu wajibu wao mahala pa kazi ili kuleta tija na kuongeza uzajishaji
Usimamizi
Kusimamia maslahi ya Wanachama katika njia ambayo itawahakikishia ustawi wao wa kitaaluma na kiuchumi