Huduma Zetu
Katika kufikia malengo ya Chama tuliyojiwekea ya kutoa huduma bora kwa Wanachama wetu (quality public services), mnamo mwezi januari 2023, Baraza Kuu Taifa lilipitisha mpango mkakati wa Chama wa miaka minne. Utakaojikita katika kuboresha huduma zetu.
Kupigania mazingira na hali bora ya kazi kwa Wafanyakazi wote
Kufanya tafiti na kuishauri Serikali kuhusu sera nzuri ya kuboresha na kuendeleza hali nzuri ya wanachama katika maisha yao wakiwa kazini.
Kuwa msemaji kwa niaba ya Wafanyakazi waliopo chini ya Serikali za Mitaa
Kulinda maslahi ya wanachama kwa kuwasiliana na Serikali ili kuepukana na uandaaji wa Sera na Sheria ambazo ni hatari kwa wanachama.
Kuendeleza ustawi wa kusimamia maslahi ya Wanachama
Kupigania na kuwahimiza waajiri kuboresha na kuendeleza hali ya wanachama katika maisha yao wakiwa kazini na wakati wa kustaafu.
Kuanzisha na kudumisha uhusiano na ushirikiano na wadau wengine
Kuendelea Kushirikiana na kubadilishana ujuzi na vyama vingine vya wafanyakazi nchini pamoja na vile vya kimataifa kwa lengo la kuboresha maslahi ya wanachama wake.
Kutoa elimu kwa wanachama kuhusu wajibu wao mahala pa kazi
Kuhimiza wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii na uadilifu wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku. Pia kuwaelimisha kuhusu Sheria, Kanuni na Taratibu zinazotumika nchini.
Kuwatetea wafanyakazi katika mashauri na kesi kazini
Kutoa huduma za kiutumishi na kisheria kwa wanachama wake pale wanapokuwa na changamoto za kesi, migogoro ama mashauri pindi wanapokuwa kazini.
