Huduma zetu

Ni muda sasa wa kujiunga na TALGWU

Katika kufikia malengo ya Chama tuliyojiwekea ya kutoa huduma bora kwa Wanachama wetu (quality public services), mnamo mwezi januari 2018, Baraza Kuu Taifa lilipitisha mpango mkakati wa Chama wa miaka minne. Utakaojikita katika kuboresha huduma zetu. 

Kulinda na kuoanisha mazingira na hali bora ya kazi kwa Wafanyakazi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa

TALGWU itajikita katika tafiti zenye lengo la kubaini uwiano wa mishahara kati ya Watumishi wa Serikali za Mitaa na sekta nyingine ili kupata msingi wa majadiliano na Mwajiri. Chama kitajenga misingi ya majadiliano ya pamoja na Serikali juu ya mishahara bora kwa Wafanyakazi, pamoja na kumshawishi Mwajiri kuboresha Ofisi wanazotumia Wanachama wetu na kutoa vitendea kazi.

Kukifanya Chama kuwa msemaji mkuu kwa niaba ya Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa kutoka ngazi ya Taifa hadi chini

ambapo Chama kitaongeza idadi ya Wanachama kutoka 67% ya wafanyakazi wote wa Serikali za Mitaa kwa sasa hadi 95% ya wafanyakazi wote wa Serikali za Mitaa ifikapo mwaka 2022 pamoja na kufikia kuwa na mbinu ya pamoja katika kushughulikia masuala yote yanayoathiri utoaji wa huduma bora kwa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa .

Kuendeleza ustawi wa kusimamia maslahi ya Wanachama katika njia ambayo itawahakikishia ustawi wao wa kitaaluma na kiuchumi

Chama kitalinda na kutetea maslahi ya Wanachama wetu katika kipindi chote cha utekelezaji wa mpango mkakati huu. Aidha Chama kitandelea kuifadhili TALGWU MICROFINANCE PLC ili iweze kukopesha Wanachama wengi zaidi pamoja na kudumisha hadhi ya ustawi wa kiuchumi na kijamii ya Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa

Kuanzisha na kudumisha uhusiano na ushirikiano na wadau wengine

ambapo Chama kitaendelea kuimarisha uhusiano uliopo kati yake na Vyama vingine vya Wafanyakazi na wadau mbalimbali ndani ya nchi, Kikanda na Kimataifa pamoja na kuendeleza na kudumisha mahusiano na mashirikiano mengine kwa maslahi ya Wanachama wetu ..

Kwanini TALGWU ?

Kwanini wafanyakazi wa Serikali za Mitaa wajiunge na TALGWU ?