• Home
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Mikakati ya Chama
  • Utawala
    • Idara
      • Idara ya Elimu, Jinsia na Uimarishaji
      • Idara ya Habari na Uhusiano
      • Idara ya Utawala na Utumishi
      • Idara ya Fedha
      • Idara ya Sheria na Usalama Kazini
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi
    • Muundo wa Utawala
  • Huduma zetu
  • Miradi
  • Picha na Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Tazama Video
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo ndogo
    • Ripoti Mbalimbali
    • Miongozo
    • Pakua Form
  • Maswali
    • Malalamiko
  • Mawasiliano
TalgwuTalgwu
    • Home
    • Kuhusu sisi
      • Historia
      • Dira na Dhima
      • Mikakati ya Chama
    • Utawala
      • Idara
        • Idara ya Elimu, Jinsia na Uimarishaji
        • Idara ya Habari na Uhusiano
        • Idara ya Utawala na Utumishi
        • Idara ya Fedha
        • Idara ya Sheria na Usalama Kazini
      • Vitengo
        • Ukaguzi wa ndani
        • Kitengo cha Manunuzi
      • Muundo wa Utawala
    • Huduma zetu
    • Miradi
    • Picha na Habari
      • Taarifa kwa Umma
      • Hotuba za Viongozi
      • Maktaba ya Picha
      • Tazama Video
    • Machapisho
      • Sheria Ndogo ndogo
      • Ripoti Mbalimbali
      • Miongozo
      • Pakua Form
    • Maswali
      • Malalamiko
    • Mawasiliano

    Mikakati ya Chama

    • Home
    • Mikakati ya Chama

    Mikakati

     

    MPANGO MKAKATI WA TALGWU KWA KIPINDI CHA MWAKA 2018 – 2022

    Katika kufikia malengo ya Chama tuliyojiwekea ya kutoa huduma bora kwa Wanachama wetu(quality public services), mnamo mwezi januari 2018, Baraza Kuu Taifa lilipitisha mpango mkakati wa Chama wa miaka minne uliojikita katika maeneo matano kama ifuatavyo:

    1. Kulinda na kuoanisha mazingira na hali bora ya kazi kwa Wafanyakazi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.

      TALGWU itajikita katika tafiti zenye lengo la kubaini uwiano wa mishahara kati ya Watumishi wa Serikali za Mitaa na sekta nyingine ili kupata msingi wa majadiliano na Mwajiri. Chama kitajenga misingi ya majadiliano ya pamoja na Serikali juu ya mishahara bora kwa Wafanyakazi, pamoja na kumshawishi Mwajiri kuboresha Ofisi wanazotumia Wanachama wetu na kutoa vitendea kazi.

    2. Kukifanya Chama kuwa msemaji mkuu kwa niaba ya Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa kutoka ngazi ya Taifa hadi chini

      ambapo Chama kitaongeza idadi ya Wanachama kutoka 67% ya wafanyakazi wote wa Serikali za Mitaa kwa sasa hadi 95% ya wafanyakazi wote wa Serikali za Mitaa ifikapo mwaka 2022 pamoja na kufikia kuwa na mbinu ya pamoja katika kushughulikia masuala yote yanayoathiri utoaji wa huduma bora kwa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa .

    3. Kuendeleza ustawi wa kusimamia maslahi ya Wanachama katika njia ambayo itawahakikishia ustawi wao wa kitaaluma na kiuchumi

      . Chama kitalinda na kutetea maslahi ya Wanachama wetu katika kipindi chote cha utekelezaji wa mpango mkakati huu. Aidha Chama kitandelea kuifadhili TALGWU MICROFINANCE PLC ili iweze kukopesha Wanachama wengi zaidi pamoja na kudumisha hadhi ya ustawi wa kiuchumi na kijamii ya Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa .

    4. Kuanzisha na kudumisha uhusiano na ushirikiano na wadau wengine

      ambapo Chama kitaendelea kuimarisha uhusiano uliopo kati yake na Vyama vingine vya Wafanyakazi na wadau mbalimbali ndani ya nchi, Kikanda na Kimataifa pamoja na kuendeleza na kudumisha mahusiano na mashirikiano mengine kwa maslahi ya Wanachama wetu ..

    5. Kujenga na kuboresha uwezo wa kitaasisi wa Chama.

      Katika kutekeleza hili, Chama kimejipanga  kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato, kuboresha usimamizi wa kimenejimenti na kiuongozi, kutoa msaada wa miundombinu utakao kiwezesha Chama kutekeleza shughuli zake za msingi ipasavyo, kuendeleza juhudi za kuwepo kwa usawa wa jinsikwenye ngazi zote za uongozi wa Chama pamoja na kuinua TALGWU Makao Makuu kufikia hadhi ya viwango vya Kimataifa ifikapo 2022.

    Search

    Categories

    • Uncategorized

    Latest News

    Ushiriki wa chama katika siku ya wanawake duniani
    11Mar2022

    Mawasiliano

    Simu: +255 738 774 775

    Barua pepe : info@talgwu.or.tz

    Anwani

    TALGWU Makao Makuu 
    Anuani ya Posta: S.L.P 16097, Dar es Salaam,
    Mtaa: Bingo St/Taifa Road- Benjamin Mkapa stadium

    Visitor Counter

    0063922
    Visit Today : 213
    This Year : 34299
    Total Visit : 63922
    Who's Online : 1

    Copyright@talgwu .@2021

    • Privacy
    • Terms
    • Account