M/Kiti Taifa Ndg. Tumain P. Nyamhokya
Ni Chama cha wafanyakazi wa serikali za Mitaa Tanzania ambacho kimesajiliwa chini ya sheria ya vyama vya wafanyakazi no 10 ya mwaka 1998, na kilipewa nambari ya usajili 010 tarehe 15/09/2000. TALGWU inaunganisha wafanyakazi wote waliopo chini ya Mamlaka za serikali za mitaa na Taasisi nyingine nchini ambapo hadi kufikia Novemba 2018, Chama kilikuwa na wanachama 64,224.
TALGWU inajishirikisha na shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) ,shirikisho la vyama vya wafanyakazi vinavyotoa huduma kwa umma duniani (PSI) na Mtandao wa Vyama vya Wafanyakazi vya Serikali za Mitaa Africa (AMALGUN). Hivyo basi chama cha wafanyakazi ni ummoja, muungano, na mshikamano wa wafanyakazi ambao nia, malengo, matakwa na matarajio yao yanafanana.
Umoja huo ndio nguzo pekee ya kupatia ufumbuzi wa matatizo yao.
TALGWU inaelimisha, inatetea, na kulinda ajira na ujira wa wanachama wake kwa kuzingatia sheria, taratibu, kanuni, miongozo na nyaraka mbalimbali za kazi.
Dhima
Kuunganisha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa kwa ajili ya kupigania uwepo wa huduma bora, uboreshwaji wa huduma za kiuchumi na kijamii, uwepo wa maendeleo endelevu ya kitaaluma na kitaalam, na kuimarisha nguvu ya pamoja ya majadiliano, ili kufikia kuwa jamii yenye usawa kupitia Uongozi bora.
Dira
Ni Kuwa Chama cha Wafanyakazi chenye ufanisi mkubwa na kinachojitegemea nchini Tanzania.



